
Usiku wa November 2 mtandao maarufu wa habari Uingereza express.co.uk uliandika maamuzi ya shirikisho la soka Uingereza FA baada ya kupatikana na hatia ya kosa la utovu wa nidhamu kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, kocha huyo amefungiwa mechi moja na FA na kutozwa faini ya pound 40,000 kwa kosa la utovu wa nidhamu alilolionesha katika mechi aliyopoteza dhidi ya West Ham United.
Kocha huyo wa Chelsea amekubali adhabu hiyo kutoka FA na atakosa mchezo dhidi yaStoke City ugenini kutokana na kosa la kuwatolea maneno mabovu waamuzi wa mchezo dhidi ya West Ham United October 24 2015 tukio ambalo lilimfanya aondolewe na muamuzi katika benchi. Hata hivyo Chelsea wamepoteza jumla ya mechi sita katika mechi zao 11 walizocheza katika Ligi Kuu msimu huu. Mourinho alitenda kosa hilo wakati wa mapumziko ya mchezo huo.
0 Response to "FA waendelea Kumuandama Jose Mourinho sasa hivi wamekuja na adhabu hii Kwa kukutwa na hatia ya kosa la utovu wa nidhamu."
Post a Comment