Baada ya kuisogeza kwetu behind the scenes ya video yake mpya, msanii wa muziki waPop R&B kutoka Marekani, Tinashe ameamua kuidonosha video ya wimbo wake mpyaPlayer feat. Chris Brown.
Player ni single ya kwanza intakayopatikana kwenye Album mpya ya Tinashe, Joyride,mbali na kushirikiana na Chris Brown kwenye wimbo huu, wasanii wengine wakubwa watakaosikika kwenye Album mpya ya msanii huyo ni pamoja na Max Martin, Dr. Luke, Hit-By, Travis Scott (ambaye pia ndiye aliyehusikia kwenye uandishi wa single hii),Young Thug na wengine kibao.
Alipoulizwa nini kilimsukuma kufanya kazi na Chris Brown, Tinashe alikuwa na haya ya kusema; >>>” Chris Brown ni mtu ambaye anakipaji kikubwa sana, cha kuimba na cha kucheza, na nilipomaliza kuingiza vocal zote nikaamua kumtafuta kuona kama angependa kuweka vocal zake pia ili kuifanya track iwe kali zaidi, akakubali”. <<<
Hapa chini nimeisogeza official music video ya Tinashe feat. Chris Brown; ‘Player’ na kama bado video hii haijagusa macho yako basi feel free kuicheki single hiyo hapa chini.
0 Response to " #CheckOut Tinashe anatusogezea kwa karibu official music video ya ‘Player’ feat. Chris Brown – (Video)!"
Post a Comment