MPENZI wa staa wa Bongo Fleva nchini, Nasibu
Abdul 'Diamond Platnumz' Zarinah Hassan 'The
Boss Lady' amemtakia heri ya kuzaliwa wifi yake
Esma kupitia akaunti yake ya Instagram huku
post yake ikizua jambo kwa mashabiki.
Zari ambaye bado yupo Bongo, katika post yake
hiyo awali aliandika 'Happy bday to my lovely
shemeji wifi' ila baadaye aliamua kubadilisha
baada ya baadhi ya mashabiki wake kumkosoa
huku wengine wakidai anatafuta kiki na baadhi
wakimtolea maneno ya kuudhi. Usahihi alitakiwa
kutumia neno WIFI na siyo SHEMEJI ambalo huwa
linatumika kwa mvulana!
Esma ni dada wa Diamond ambaye ameolewa na
Petiti Man.

0 Response to " ZARI AZUA BALAA INSTAGRAM BAADA YA KUPOST KIUCHOKOZI"
Post a Comment