Na Makongoro Oging’ /Uwazi
MFANYABIASHARA tajiri Afrika Mashariki na
Kati, Said Salum Bakhresa (pichani ) , jina lake
limetumika katika utapeli jijini Dar baada ya
watu waliodai ni wafanyakazi wake kumrubuni
mkazi wa Kariakoo , Mussa Mohammed
kuvunja fremu yenye duka lake ili kupisha
ujenzi wa maegesho ya magari , Uwazi
limedokezwa.
Mfanyabiashara tajiri Afrika Mashariki na Kati ,
Said Salum Bakhresa.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni
katika jijini Dar, Mohammed alisema
wafanyakazi hao waliodai kutumwa na tajiri
huyo, walimwambia baada ya kuvunja , duka
jipya lingejengwa ndani ya siku kumi.
“ Nilikataa kwani niliona siku kumi kukaa bila
kufanya biashara ni nyingi na isitoshe yeye
siyo mwenye duka nililopanga , hata hivyo ,
msimamizi wa mwenye nyumba
walionipangisha, Juma alinisihi nikubali kwa
vile wana nia nzuri , nilitoa vyombo nje ,
nikavifunika kwa turubai nikisuburi siku hiyo
ya kujengewa .
“ Siku kumi zilipita bila kunijengea duka , alikuja
kwangu tena Huzefa akaniambia mzee
Bakhresa amesema hapatajengwa tena kwani
eneo ni lake, nilichanganyikiwa nikijiuliza
fedha nilizokopa benki na kwa watu
nitazirudishaje .
“ Nilifunga safari mpaka kwa Bakhresa na
kumwelezea, akanipa pole na kuniambia
hapatajengwa kwa madai eneo ni la kwake ,
akanishauri nishirikiane na Omari kutafuta
fremu nyingine ya biashara atalipia.
“ Akaniambia tukishapata fremu malipo
yatafanyika kupitia kwa Omari , kwa bahati
nzuri tukapata sehemu Kariakoo ambapo kodi
kwa mwezi ni milioni moja na nusu, walisema
niandike kwa maandishi , nikafanya hivyo ,
ilikuwa ni kwa muda wa mwaka mmoja sawa
na shilingi milioni kumi na nane .
“ Nilimpa Omari akampelekea lakini mpaka
sasa sijapata jibu na nikiomba nimuone
Bakhresa hawataki , wananifukuza, nikimpigia
Omari simu hapokei , akipokea ananijibu
vibaya ingawa yeye ndiye aliyeambiwa
atamaliza kila kitu, nimekuwa kama adui .
Bw . Mussa Mohammed anyedai kurubuniwa
na watu waliodai kuwa ni wafanyakazi wa
Bakhresa.
“ Siku moja nilikutana na Omari nilimuulizia
akasema mzee amesema atanipa milioni moja
tu na siyo kwa sasa, nilijisikia vibaya kwani
nanyeshewa mvua hapa nje , familia yangu
inateseka , watoto wangu hawasomi,
nashindwa kurejesha mkopo, mali yangu
inaharibika wao hawajali, nataka nimuone
Bakhresa uso kwa uso maana inawezekana
ameshatoa fedha ikaliwa na wajanja, ” alisema
Mohammed .
Msimamizi wa mwenye nyumba iliyokuwa na
duka la Mohammed , Juma alikiri kwamba
duka lililovunjwa lipo katika eneo lao na hata
kodi walikuwa wanalipwa wao , akidai suala
hilo ni la kibabe na ameahidi kumtafuta
Bakhresa ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.
Omari alipotafutwa kwa njia ya simu alisema
suala hilo analijua na mzee Bakhresa ndiye
aliyemtuma alisimamie na kwamba kuhusu
malipo mlalamikaji hatapata chochote kwa vile
eneo lile ni la Bakhresa.
Hata hivyo , gazeti hili bado linahitaji
kujiridhisha ili kujua kwa nini Bakhresa
anatajwa mara kwa mara wakati kiuhalisia ,
baada ya duka hilo kuvunjwa kwa ushauri wa
mmiliki wake , ambaye ndiye aliyekuwa
akilipwa kodi ya pango na mlalamikaji, ndiye
aliyepaswa kulalamikiwa na Mohammed .
Kwa mujibu wa Mohammed , alilipa kodi ya
mwaka mmoja kwa mwenye nyumba huyo ,
ambaye hata hivyo , hasemi lolote juu ya
madai ya wapambe wa Bakhresa wanaodai
eneo hilo ni la mzee huyo tajiri . Uwazi
linafuatilia kwa karibu sakata hili .

0 Response to "HII HATARI !!! BAKHRESA ATUMIKA KUTAPELI WATU"
Post a Comment