Unakumbuka mwaka 2009 pale Kanye West alipowashangaza watazamaji baada ya kumnyakua mic Taylor Swift kwenye tuzo za MTV?
Kidogo itokee tena. Tunafahamu kuwa Kanye ni shabiki mkubwa wa Beyonce na usiku wa kuamkia leo kwenye tuzo za Grammy alitaka kurudia kuuonesha ulimwengu namna alivyo shabiki namba moja wa Bey.
Kipengele cha Album of The Year kilienda kwa msanii wa rock aitwaye Beck na kumshinda Beyonce aliyekuwa akiwania pia.
Wakati Beck alipokuwa akishukuru kupata tuzo hiyo Kanye alipanda jukwaani kutaka kumkatiza lakini akaashia kumshika mkono kuashiria kuwa alikuwa akitania tu.
Tazama video hapo juu.
0 Response to " Grammys: Kanye West atania kumkwapua mic msanii mwingine (Video)"
Post a Comment