Latest Updates

Unashangaa ushirikina katika soka la bongo? Angalia huu wa mashabiki wa TP Mazembe kwenye fainali (+Audio)





Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumapili ya November 8 itacheza mchezo wake wa pili wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na USM Alger yaAlgeria mjini Lubumbashi. TP Mazembe watacheza mchezo huo wa pili wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga USM Alger katika mchezo wa kwanza uliyochezwaAlgeria kwa jumla ya goli 2-1.


Wachezaji wa TP Mazembe wakiwa kanisani

Kuelekea mchezo huo klabu ya TP Mazembe wamefanya kitu tofauti kidogo na timu nyingi za Afrika ambazo tumezoea kuona zikihusishwa na imani za kishirikina, hususani zikiwa zinaelekea katika mechi ngumu kama hiyo, TP Mazembe walikusanyika na mashabiki wao na mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi Chapwe na kwenda pamoja kufanya ibada kanisani ili kuomba mungu wapate matokeo mazuri.


Moise Katumbi Chapwe akiwa mbele ya mchungaji wa kanisa ambalo huwa wanasali kuelekea katika mechi zao

Kitendo walichofanya TP Mazembe inaripotiwa kuwa huwa ni kawaida yao kufanya ibada hususani wakiwa wanaelekea katika mchezo mgumu, hii inashangaza kidogo kwani kwa kumbukumbu za karibuni haijawahi kufanywa na klabu za Tanzania zaidi ya kusadikiwa kufanya ushirikina katika mechi zao.



Hii ni sauti ya ibada hiyo waliofanya TP Mazembe na mashabiki wao

0 Response to "Unashangaa ushirikina katika soka la bongo? Angalia huu wa mashabiki wa TP Mazembe kwenye fainali (+Audio)"

Post a Comment