Klabu ya FC Barcelona usiku wa October 17 ilishuka dimbani kucheza mechi yake ya Ligi Kuu Hispania kwa kuwakaribisha Rayo Vallecano katika uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou. Licha ya FC Barcelona kushuka dimbani bila nyota wake Lionel Messiambaye anauguza jereha la mguu wake, FC Barcelona imeibuka na ushindi.
FC Barcelona imeibuka na ushindi mnono tofauti na wengi walivyotegemea kwani kumkosa nyota wake Lionel Messi kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kudhoofisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika, klabu ya FC Barcelona iliibuka na ushindi wa jumla ya goli 5-2.
Neymar ndio aliibuka nyota wa mchezo huo kwa kufunga magoli manne kati ya matano,Neymar dakika ya 22 na 32 alifunga goli mbili kwa mikwaju ya penati kabla ya dakika ya 69 na 70 kufunga magoli mengine mawili, mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarezalihitimisha idadi ya magoli matano kwa kufunga goli dakika ya 77. Rayo Vallecanolicha ya kuwa wa kwanza kufunga goli wameishia goli 2 zilizofungwa na Javi Guerradakika ya 15 na Jozabed dakika ya 86.
Matokeo ya mechi nyingine za Laliga zilizochezwa October 17
Video ya magoli ya FC Barcelona Vs Rayo Vallecano
0 Response to "#Usipitwe na Full Time ya FC Barcelona Vs Rayo Vallecano na mechi nyingine za Ligi Kuu Hispania Oct 17! (+Video)"
Post a Comment