Latest Updates

#UmeipataHii Uongozi wa MDB waweka wazi ‘mkuki wa moyoni’ waliochomwa na Young Dee na Kusema kuwa Dogo amepotea..Hii ndo hali aliyonayo sasa.






Uongozi wa Millian Dollar Boys unaomiliki studio za Authentic za jijini Dar es Salaam umesikitishwa na kitendo cha ukosefu wa fadhila na shukrani, kilichofanywa na rapper Young Dee aliyekuwa chini yake.


Millian

Hivi karibuni Young Dee alidai kuwa uongozi huo pamoja na mambo mengine ulimzuia kuwa member wa kundi la Mtu Chee.

CEO wa kampuni hiyo, Millian, amedai kuwa Young Dee amesahau wema waliomtendea kiasi cha kuanza kuongea maneno ya dharau yanayowaumiza roho.

“This is how I feel about this,” ameandika kwenye Instagram.

Ulipokuwa huna nilikuona, nikakuhurumia na kukusaidia. Sikuwahi kukudai pesa hata shilingi moja kwa yote nilokusaidia. Nilikutungia nyimbo Ambazo zilikurejesha kwenye chati na kukupa heshima kubwa sana. Nyimbo Ambazo mwanzo hukuzielewa lakini baada ya kuziachia zimekuwa Ndo nyimbo zako pekee kali zinazotamba hadi hii leo. Nilikukaribisha nyumbani kwangu, hata kudiriki kuwahamisha baadhi ya Watu ili wewe upate chumba cha kujisitiri. Na hata ulipoamua kuhama sio kwamba nilikufukuza,” aliongeza.

“Ulitamani uhuru wa kukaa peke yako ili uweze kufanya Yale uyapendayo. Na hata ulivyoamua hivyo bado nilikujali, na kukilipia kodi chumba kipya ulichokipata. Mara nyingi ulisanda na kutamani kurudi nyumbani, ahadi yangu ikabaki palepale kwamba kwangu Ni nyumbani kwako. Ulikuja mara nyingi japo kula chakula. Mara ya Mwisho nakumbuka kodi niliyokulipia iliisha, ukakosa pa kuishi watu wakakuita Yahaya. Popote usiku mnene ulipokukuta ndipo ulipoangusha, hukuona tena umuhimu hata wa kutafuta kwako.”

“Ulevi ukaendeleza tena uliopindukia, habari zikaanza enea kwamba unabuya unga. Hayo uliyakana kwa nguvu zako zote, lakini popote ulipoonekana watu walinukuu. Kwa Upendo tulikuita uvumi kuuchunguza, yetu ukayapuuza na kufanya yaliyo yako. Inaniuma hadi mtimani, kuona unapotea, lakini Mola ajua Ni Mara ngapi nimejaribu.”

Kwenye maelezo mengine, Millian amesema, “Ni Nani utakayemlaumu kwa umasikini wako? Ni nani aliyekwambia uyaache yaliyo ya maendeleo na kujiingiza kwenye magenge ya wahuni? Kama usiposhtuka sasa hivi na kugundua kuwa huna hata chumba cha kupanga au hata begi la nguo Halafu unajiita Msanii wa muziki utastuka when it’s very late. Washkaji zako wote ni wahuni, bangi, cocaine, pombe na madem wasiojua hata kuandika aeiou. Hayo sio maisha! Nimekuonyesha njia ukaniona bwege. I am not responsible for your downfall. And if you don’t know, you’re about to hit rock bottom. Get up before we lose another very potential artist.”

0 Response to "#UmeipataHii Uongozi wa MDB waweka wazi ‘mkuki wa moyoni’ waliochomwa na Young Dee na Kusema kuwa Dogo amepotea..Hii ndo hali aliyonayo sasa."

Post a Comment