Wakati kukiwa na mfululizo wa stori za Siasa kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchi nzima, yani Tanzania bara na visiwani Zanzibar siku yaOctober 25 2015, imekuja taarifa ya tofauti toka Zanzibar kuhusu uchaguzi huo ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha alitangaza kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi huo kwa upande wa Zanzibar !!
Mwenyekiti huyo amekutana na Vyombo vya habari na kutoa ufafanuzi sababu za Tume hiyo kufuta matokeo hayo.
“Baadhi ya Wajumbe badala ya kuwa Makamishna wa Tume, wamekuwa wawakilishi wa vyama vyao… kumegundulika kasoro nyingi katika Uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kugundulika kwa baadhi ya vituo vimekuwa na Kura nyingi zaidi kuliko daftari wa wapiga Kura…“- Hii ni nukuu ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha.
“Taarifa iliyowasilishwa na Wajumbe wetu waliowakilisha Tume Pemba, kulifanyika uhamishaji wa Masanduku ya kupigia Kura na kuhesabiwa kwenye maeneo nje ya vituo vya kupigia Kura kinyume na taratibu…“
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha.
“Kuna vijana walivamia vituo na kufanya fujo kuzuia watu na kuzuia wengine kupiga Kura… Kuna vyama vya Siasa viliingilia majukumu ya Tume na kujitangazia ushindi na kupeleka mashinikizo kwa Tume… pia kulikuwa na malalamiko ya vyama mbalimbali kutoridhika na mchakato wa kupiga Kura, kuhesabu na matokeo.”- Jecha Salim Jecha.
“Kuna namba za Fomu za matokeo zilionekana kufutwa na kuandikwa upya namba nyingine juu yake… kwa kuzingatia hayo, nimeridhika kwamba Uchaguzi haukuwa wa haki na kumekiukwa Sheria na taratibu za uchaguzi… Natangaza Uchaguzi huu na matokeo yake umefutwa, kuna haja ya kufanyika uchaguzi mwingine. ” >>>- Jecha Salim Jecha.
Hii hapa sauti yote ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jechaakiongelea hayo yote.
0 Response to "#Uchaguzi2015 Haya ndio Mambo tisa yaliyofanya matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar kufutwa… (Audio)"
Post a Comment