Latest Updates

PICHA ZA MAFURIKO YA AJABU YA LOWASSA HUKO TANGA,WATU ZAIDI YA 50 WAZIMIA,MKUTANO WAAHIRISHWA



Wananchi waliolazwa chini baada ya kuzimia ni ndani ya mkutano ulioahirishwa Tanga uwanja ulikuwa mdogo sana..





Kampeni za mgombea urais kupitia ukawa zilizokuwa zifanyike Tanga jana zimeahirishwa kutokana na msongamano mkubwa sana wa watu ambao wamekuwa wakibanana na kukosa hewa na kupelekea watu kupoteza fahamu.

Mkutano huo umeahirishwa ili watu wasiendelee kufurika. Na hii ni baada ya watu zaidi ya 50 kuzimia




















Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa amelazimika kuahirisha mkutano mjini Tanga baada ya maelfu ya wakazi waliojitokeza kushindwa kuenea ndani ya uwanja wa Tangamano jijini Tanga
Kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Tanga shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5,6,7, 8 zililazimika kusimama kwa muda baada ya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliojitokeza katika uwanja wa Tanagmano, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea kwa mkutano huo.
Licha ya juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo kushindikana jambo lililomlazimu Mh.Edward Lowassa kulazimika kusitisha mkutano huo.
Je? Nini kauli ya Chadema baada ya mkutano huu kuvunjika, John Mrema ni meneja kampeni wa Chadema.
Umati huo wa wakazi wa jiji la Tanga ulionekana dhahili ulionekana dhahili kuwashinda maafisa wa taasisi ya mslaba mwekundu redcross mjini Tanga.
Akiwa jiji Tanga katika siku yake ya kwanza ya kampeni alifanya mikutano katika maeneo ya Bumbuli Mombo kabla ya kuhitimisha katika uwanja wa Tanagmano mjini Tanga ambapo aliahidi kuboresha sekya ya afya ndani ya siku miamoja baada ya kuapishwa.

0 Response to " PICHA ZA MAFURIKO YA AJABU YA LOWASSA HUKO TANGA,WATU ZAIDI YA 50 WAZIMIA,MKUTANO WAAHIRISHWA"

Post a Comment