Mrembo na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu amefunguka na kusema kwasasa amepoa na kunavitu vingi anataka kuvifanya ikiwemo kutaka kuolewa.
Mwnadada Wema aliyasema hayo kwenye kipande kidogo cha video ambacho kinasambaa mtandaoni, kikiwaonyesha Wema na meneja wake Martin Kadinda, ambapo Kadinda anamuuliza Wema kwanini siku hizi amepoa sana, na ndipo Wema akamjibu kwa kuwa anavitu vingi anataka kufanya na sasa hivi kwani anataka kuwa mke wa mtu. Ipo hivi;
Kadinda alimuuliza Wema, “mbona siku hizi umepoa sana?”
Wema akajibu huku akitabasamu na kwa shauku kubwa akasema “Sasa hivi amepoa,unajua kuna vitu vingi nataka kufanya”.. akaangua kicheko kidogo na kisha akamnong’oneza Kadinda na kumwambia “ anataka kuolewa”
Hata hivyo Wema alisita kumweka wazi mwanaume anayetaka kumweka ndani na kumtaka meneja wake kuwa na subira.
0 Response to " Wema: Kwasasa Nimepoa, Nataka Kuolewa!!"
Post a Comment