Kamba iliotumiwa kumnyonga Saddam kuuzwa kwa zaidi ya dola millioni 4
Kamba iliotumiwa kumyonga aliyekuwa rais wa Iraq Marehemu Saddam Hussein kuuzwa
Kamba iliotumiwa kumyonga aliyekuwa rais wa Iraq marehemu Saddam Hussein imedaiwa kuuzwa kwa zaidi ya dola millioni 4.
Licha ya Saddam kunyongwa mwaka 2006,watu bado wanamuenzi na mtu mmoja amejitolea kulipa dola millioni 7 kununua kamba hiyo iliokatiza maisha ya kiongozi huyo wa zamani.
Kulingana na gazeti la Metro,Baadhi ya watu matajiri wanaoitaka kamba hiyo wanatoka mataifa ya Kuwait,Iran na Israel.
Kamba hiyo kwa sasa inamilikiwa na Dr Mowaffak al-Rubaie,mshauri wa usalama wa zamani nchini Iraq,ambaye aliongoza eneo ambalo rais huyo wa zamani aliuawa.
Aliamua kuihifadhi kamba hiyo baadaye na sasa anataka zaidi ya dola millioni 7 kuiuza kamba hiyo.
Posted by Astalavista
on Saturday, February 7, 2015,
Add Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Response to " Kamba iliotumiwa kumnyonga Saddam kuuzwa kwa zaidi ya dola millioni 4"
Post a Comment