Kaka huyo ambaye anaitwa Wang aliamua kumchoma kisu dada yake kutokana na kutopendezwa na usumbufu anaofanyiwa mama yake huo, ambapo dada huyo alifariki.
Wang muda mwingi hukaa nyumbani kumhudumia mama yake na kufanya kazi zote za nyumbani, ikiwemo kupika na kufanya usafi lakini dada yake hakuwa msaada wowote kwa mama yake, ni mtu wa kushinda na rafiki zake.
Baada ya kufanya mauaji hayo alishafisha eneo hilo, akamuandalia mama yake breakfast na chakula cha mchana, baada ya mama yake kupumzika Wang aliwaita Polisi na kukiri kuhusika na tukio hilo kutokana na kuchoshwa na matatizo ya nyumbani kwao na kudai kuwa dada yake mara nyingi amekuwa akimuonea mama yao ikiwemo kumdai fedha kila siku na kwenda kutumia na rafiki zake.
0 Response to "Baada ya kuchoshwa na uonevu unaofanywa kwa mama yake, jamaa aamua kumfanyia ukatili dada yake…"
Post a Comment