‘Koko Master’, D’Banj mtu mkubwa kwenye muziki anayeiwakilisha Nigeria na Afrika kwenye ramani ya dunia hakika anajivunia mengi kwenye safari yake, mafanikio ya kufanya kazi na lebo ya GOOD MUSIC ya Kanye West ni zawadi kubwa kwake kwenye hii miaka kumi.
Juzi January 31 kafanya party Lagos, Nigeria, staa mwanamitindo kutoka Marekani ambaye alikuwa mpenzi wa Rapper Wiz Khalifa, Amber Rose unambiwa alishuka zake Lagos Naija, kumpa shavu Banj kwenye celebration ya miaka 10, Amber alikuwa MC kwenye event hiyo.
Amber Rose na D’Banj muda mfupi baada ya Amberkuwasili Nigeria.
Amber Rose baada ya kuwasili Nigeria.
Shaydee, Banky W, Ifeanyi Nwune ni baadhi ya mastaa waliojitokeza kwenye party hiyo.
Amber Rose na D’Banj, mbele zinaonekana baadhi ya Tuzo alizowahi kushinda staa huyo.
Kwenye stage Amber Rose hapa alijaribu kucheza Shoki wimbo wa Kesh, staa wa Nigeria
Huu ni wimbo wenyewe wa Kesh ft. Davido & Olamide, Unaitwa Shoki
0 Response to " Amber Rose ndani ya Nigeria kwenye party ya miaka 10 ya D’Banj kwenye muziki… (PICHAZ &VIDEO)"
Post a Comment